Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya amani ya Mali yasisitizwa kwenye Umoja wa Mataifa

Makubaliano ya amani ya Mali yasisitizwa kwenye Umoja wa Mataifa

Pande zote zinapaswa kusitisha mapigano nchini Mali, amekariri Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mchakato wa amani nchini Mali uliofanyika alhamis kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Eliasson ameongeza kuwa makubaliano yaliyosainiwa mjini Algiers, Algeria baina ya pande za mzozo ni ukomo wa utaratibu mrefu akisisitiza umuhimu kwa kuyatekeleza bila kuchelewa.

Aidha amesisitiza umuhimu kwa serikali wa kutekeleza mabadiliko ya utawala yaliyotarajiwa, kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na kupambana na ukwepaji wa sheria, akizingatia ushirikishwaji wa wanawake.

Hatimaye ametoa wito kwa wafadhili waisaidie Mali ili kutimiza mahitaji ya nchi hiyo katika kujijenga upya na kuleta maendeleo kaskazini mwa nchi.