Tunafanya kila liwezekanalao watoto wakimbizi wa Syria waende shule: Brown

Tunafanya kila liwezekanalao watoto wakimbizi wa Syria waende shule: Brown

Juhudi za makusudi zinafanyika kuhakikisha watoto wakimbizi milioni mbili wa Syria ambao wako Uturuki, Lebanon na Jordan wanaenda shule amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Brown amesema wengi hawakomashuleni nahawtarajii kujiung aikiwa hawatapata usaidizi kufuatia mgogoro unaedleela kuikumbe Syria.

Amesema mbalina kukosa elimuambayo ni haki yao, watoto hao wakimbizi wako hatarini kutumikishwa katika ajira, usafirishwaji haramu, n ahata ndoa za mapema ambapo mjumbe huyo maalum wa elimu ana anasema..

(SAUTI BROWN)

‘‘Ni elimu ndiyo inayowapa vijana tumaini ili wawaeze kupanga kwa ajili ya mustakaballi wao, kujiandaa na hata kuwa na taaluma na ndiyo maana ni muhimu kuwa pamoja na kutoa misaada ya kuokoa maisha kama vile chakula, malazi na huduma za afya , tunapaswa kadri inavyowezekana kuandaa sehemu za kuwapa elimu katika kukanda wao. ‘’

Bwana Brown ametumia mkutano  huo kutangaza kuwa kamisheni ya kimataifa ya elimu na fursa imepata mjumbe mpya ambaye ni Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na tume hiyo  ripoti yao itawasilishwa ripoti  yake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwakani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF Anthony Lake aliyedhuria mkutano huo amesema haiwezekani kutimiza lengo namba nne la elimu ya msingi kwa wote ikiwa nusu ya watoto ambao wanahitaji misaada ya dharura hawatafikiwa.