Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shukrani jamii ya kimataifa kwa kutuondoa kwenye zahma Burkina Faso: Rais Kafando

Shukrani jamii ya kimataifa kwa kutuondoa kwenye zahma Burkina Faso: Rais Kafando

Rais wa serikali ya mpito nchini Burkina Faso, Michel Kafando amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo jijini New York, Marekani wakati wa mjadala wa wazi na kuomba jamii ya kimataifa kuendeleza jitihada zake za kuhakikisha kuwa demokrasia ya dhati nchni mwake.

Amesema hayo kwa kuzingatia kuwa tarehe 16 mwezi uliopita serikali ya mpito ilipinduliwa na askari wa kikosi cha ulinzi wa rais ambapo yeye pamoja na waziri mkuu na mawaziri wengine wawili walitiwa korokoroni kwa siku kadhaa.

Rais Kafando amesema kitendo cha yeye kuwepo leo New York na kuhutubia mbele ya hadhira ya Baraza Kuu kinatokana na ushirikiano wa jamii ya kimataifa uliowezesha serikali ya mpito kurejea madarakani.

Amelaani vikali mapinduzi yaliyotokea nchini mwake akiita ni ya kikatili na hivyo kusiti jamii ya kimataifa iwe pamoja na nchi hiyo hadi itakapoendesha chaguzi zake kwa huru na haki siku chache zijazo.

Katika hotuba yake Rais Kafando amegusia masuala mengine ikiwemo  hali mashariki ya kati na Marekani kuondoa vikwazo vyake dhidi ya Cuba.