Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya kemikali isifanye ulaghai katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu- UNEP

Sekta ya kemikali isifanye ulaghai katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu- UNEP

Inawezekana kufikia malengo kabambe ya maendeleo endelevu, lakini kufanya ulaghai kama ule wa kampuni ya kuunda magari ya Volkswagen hakukubaliki.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Shirika la Mpango wa Mazingira, Achim Steiner, ambaye ametaja vitendo vya kampuni hiyo kutoa takwimu za uongo kuhusu uzalishaji wa hewa chafuzi kama sakata kubwa.

Bwana Steiner amesema hayo mwishoni mwa kongamano la nne kuhusu udhibiti wa kemikali mjini Geneva, ambapo amesema ni muhimu kutafakari kuhusu jinsi kemikali zinavyoundwa na zinavyotumiwa, ili kutimiza malengo kabambe ya maendeleo endelevu.

Hata hivyo, amesema tukio hilo linaweza kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa kuuamsha ulimwengu kuhusu ubora wa hewa katika sekta ya kutengeneza magari.