Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sauti za Marais kuhusu utekelezaji wa SDG's

Sauti za Marais kuhusu utekelezaji wa SDG's

Hatimaye, ndoto ya kusongesha mbele malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs yaliyofikia ukomo mwaka huu imetimia. MDGs ililenga mathalani kupunguza kwa asilimia 50 watu wanaoshi kwa kutumia chini ya dola Moja na senti 25 kwa siku ifikapo mwaka 2015. Umoja wa Mataifa ukasema kuwa haitoshi kuishia nusu ni lazima kukamilisha kazi kwa kuwa na malengo mengine yatakayosengesha mbele ajenda hiyo. Na ndipo yakazaliwa malengo ya maendeleo endelevu, SDG  yakiwa na malengo 17 na yenye malengo madogo madogo 169.

Je viongozi wa Afrika walioshiriki kwenye uridhiaji wa malengo hayo yajulikanyo pia kama ajenda 2030 walisema nini? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii ya wiki.