Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Kagame wajadili mabadiliko ya tabianchi

Ban na Kagame wajadili mabadiliko ya tabianchi

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda ambapo wawili hao wamejadili masuala kadhaa ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Bwana Ban ametumia fursa hiyo kupongeza kupitishwa kwa malengo hayo akimsihi Rais Kagame asongeshe mbele utekelezaji wa SDGs kama alivyofanya kwenye malengo ya maendeleo ya milenia.

Kuhusu mkutano ujao wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Paris, Ufaransa mwezi Disemba, Bwana Ban amemuomba Rais Kagame kusaidia kuchagiza nchi  Afrika ili kutangaza rasmi viwango watakavyopunguza katika utoaji wa gesi chafuzi.

Halikadhalika wamezungumzia usaidizi wa Umoja wa Mataifa na jinsi ya kushughulikia mizozo kwenye ukanda wa maziwa makuu ambapo Katibu Mkuu amerejelea azma yake ya kuhakikisha suluhu inapatikana kwa njia ya amani.