Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 500 wauawa Yemen ndani ya miezi sita: UNICEF

Watoto 500 wauawa Yemen ndani ya miezi sita: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema nchini Yemen mapigano yanayoendelea yamesababisha vifo vya watoto wapato Mia Tano katika kipindi cha miezi sita pekee huku wengine 702 wakijeruhiwa. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

UNICEF inasema kama hiyo haitoshi, zaidi ya watoto zaidi milioni Moja nukta Saba wana utapiamlo huku watoto Milioni 10, sawa na asilimia 80 ya wanachi wenye umri wa chini ya miaka 18 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Halikadhalika, UNICEF inasema kila uchao, watoto wanashuhudia ndoto na matumaini yao yakitumbukia nyongo bila kufahamu mustakhbali wao.

Christophe Boulierac ni Msemaji wa UNICEF

(SAUTI Boulierac )

‘‘Kwa wastani watoto wanane kwa siku wameuwawa au kuachwa na ulemavu wa maisha tangu kuanza kwa machafuko miezi sita ilyopita. Utumikishwaji wa watoto umeongezeka kwa kasi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo watoto 156 walitumikishwa katika vikundi vyenye silaha, ilihali mwaka huu hadi sasa idaidi imefikia 656  na hivi ni visa vilivyothibitishwa.’’