Kipaumbele hivi sasa Burundi ni maendeleo: Makamu Rais Burundi

Kipaumbele hivi sasa Burundi ni maendeleo: Makamu Rais Burundi

Kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikiendelea hapa mjini New York, Marekani, Makamu wa pili wa Rais wa Burundi Joseph Butore amehutubia akimulika jitihada za serikali za kukuza mazungumzo jumuishi na maridhiano nchini humo baada ya vurugu zilizotokea kabla ya uchaguzi uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Punde baada ya hotuba hiyo, Idhaa hii ilizungumza na Alain Aimé Nyamitwe, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Burundi, akieleza ni wapi nchi yake inaweka kipaumbele sasa katika maswala ya maendeleo.

(Sauti ya waziri Nyamitwe)

Aidha amezungumzia utekelezaji wa makubaliano ya amani na maridhiano yaliyosainiwa Arusha mwaka 2000.

(Sauti ya waziri Nyamitwe)