Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yapongeza UNMISS lakini yataka mashauriano kuhusu hatma ya UNMISS

Sudan Kusini yapongeza UNMISS lakini yataka mashauriano kuhusu hatma ya UNMISS

Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Sudan Kusini, James Wani Igga amepongeza juhudi za  ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS nchini humo tangu harakati za uhuru hadi baada ya uhuru wake mwaka 2011.

Hata hivyo, Wani Igga amesema kuongezwa upya kwa mamlaka ya UNMISS bila ya mashauriano ya dhati na kina na serikali ya Sudan Kusini si sahihi na haikubaliki, kwani ni ukweli ulio wazi kwamba suala kama hili ni swala la taifa huru na mashauriano ni ya muhimu.

Wani Igga amesema hayo wakati wa hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Kuhusu makubaliano ya amani iliyotiliwa saini hivi majuzi, makamu huyo wa Rais amesema

Kwa hakika makubaliano haya ya kusitisha mapigano yana mashiko katika baadhi ya maeneo na si kote. Hii ni kwa sababu ya kukosekana kwa utaratibu wa pamoja wa kufuatilia na kuthibitisha hali ilivyo mashinani”

Na kwa maantiki hiyo, ameisihi mamlaka ya IGAD..

Kuongeza kasi ya kujenga na kuunda chombo hiki muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano hayo ya kusitisha mapigano. Kuhusiana na  mipango ya usalama, tangu tarehe 13 hadi 18 Septemba  pande kinzani zilifanya warsha iliyomalizika  kwa serikali yetu kutia saini muhtasari wa kikao lakini ndugu zetu upande mwingine walikataa kutia saini kwa sababu ambazo wao wanafahamu vizuri zaidi. Sasa ni jukumu la IGAD na mataifa mengine kuwashawishi kwa kutumia njia zozote”