Mataifa yaliyo na wakimbizi na wahamiaji wengi yasaidiwe kubeba mzigo huo

Mataifa yaliyo na wakimbizi na wahamiaji wengi yasaidiwe kubeba mzigo huo

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres, amesema mashirika ya kibinadamu na nchi zinazobeba mzigo mkubwa wa janga linaloendelea la wakimbizi na wahamiaji zinapaswa kusaidiwa zaidi, hii ikiwa ni pamoja na fedha zinazohitajika.

Guterres ametoa kauli hiyo alipohojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu  uhamiaji uliofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ambapo nchi wanachama zilijadili changamoto na majukumu , sawa na fursa , zinazoletwa na wahamiaji na wakimbizi.

Kwa maantiki hiyo, Guterres anatoa wito…

(Sauti ya Gutteres)

"Kuimarisha ushirikiano wa dhati na wa maendeleo kwa nchi ambazo zinahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi. Hususan nchi za kipato cha kati kubadili sheria ambazo zitaelekeza hatua za Benki ya Dunia na taasisi nyingine za kifedha za kimataifa , ili kuruhusu nchi hizo kama vile Lebanon, Jordan, Uturuki , Kenya , Cameroon kunufaika na mikopo nafuu na misaada"