Skip to main content

Amani na usalama ndiyo misingi ya maendeleo endelevu- Rais Rajaonarimampianina

Amani na usalama ndiyo misingi ya maendeleo endelevu- Rais Rajaonarimampianina

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeingia siku yake ya nne leo Alhamis hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo, ikiwa ni siku ya mwisho marais kuhutubia, kwa mujibu wa ratiba. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Miongoni mwa waliohutubia Baraza Kuu leo ni Rais  wa Madagascar, ambaye amesema kuwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hayawezi kutimizwa bila kuimarisha amani na usalama.

Rais Rajaonarimampianina amesema vita na ukosefu wa usalama huchangia pakubwa katika ukiukaji wa haki za binadamu, akiongeza kuwa usalama wa watu wote unapaswa kudumishwa ili nchi ziweze kuwaondoa watu wao katika umaskini.

“Sote tunajua kuwa hapawezi kuwepo maendeleo ya ukweli bila amani na usalama endelevu. Uhalifu kwenye mitandao ya intaneti, uhalifu wa kimataifa wa kupangwa, na ugaidi, vinaendelea kuwa masuala ya kuzingatiwa. Tunapaswa kuwa na mikakati ya kukabiliana na matishio haya. Usalama wa watu wetu ni lazima uhakikishwe ili tuwaokoe kutokana na hatari na umaskini.”