Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani CAR yajadiliwa na UM wakati vurugu inatishia utaratibu wa mpito

Amani CAR yajadiliwa na UM wakati vurugu inatishia utaratibu wa mpito

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo kando ya mjadala wa wazi kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR viongozi wakijadili vurugu iliyoibuka hivi karibuni. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Akihutubia mkutano huo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema mashambulizi dhidi ya raia yaliyotokea mjini Bangui ni tishio kwa utaratibu wa mpito.

Aidha Bwana Ban amemulika mafanikio yaliyopatikana hadi kufikia kongamano la maridhiano la Bangui na kuelekea uchaguzi mwisho wa mwaka huu, akipongeza Rais wa mpito Catherine Samba-Panza kwa uongozi wake.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa.

(Sauti ya Ban)

« Yaliyotokea kwa kipindi cha siku chache zilizopita, yanaoneysha umuhimu wa usaidizi wa jamii ya kimataifa, pia kupunguza tofauti za kidini na kikabila na kupata maelewano. Bado changamoto ni nyingi, siyo kwa upande wa usalama wa sasa hivi tu. Kujenga upya nchi na kupata maridhiano na mabadiliko katika nchi iliyokumbwa na mizozo kwa miaka kadhaa kunachukua muda. »

Rais wa CAR Catherine Samba-Panza naye amehutubia mkutano huo kwa njia ya video kutoka Bangui.