Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yasifu Nepal kwa kutambua haki ya chakula kupitia katiba

FAO yasifu Nepal kwa kutambua haki ya chakula kupitia katiba

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limekaribisha hatua ya Nepal kujumuisha haki ya chakula kwenye katiba ya nchi hiyo na hivyo kutambuliwa kuwa ni haki ya msingi ya kila mwananchi.

Mwakilishi wa FAO nchini Nepal Somsak Pipoppinyo amesema hatua hiyo ni ya kihistoria na itachagiza mpango wa kutokomeza njaa kwa kuzingatia lengo la kushughulikia ukosefu wa uhakika wa chakula kwenye wilaya 30 nchini Nepal hususan maeneo ya mlimani.

FAO imesema katiba yenye kipengele hicho cha haki ya chakula ilipitishwa na wabunge 507 kati ya 601 na tayari Rais Ram Baran Yadav ameshaizindua.

Ibara ya 36 inataja haki ya chakula kwa kila mwananchi na kwamba kila mwananchi anapaswa kulindwa dhidi ya uhaba wa chakula unaoweza kutishia uhai wake.