Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wahanga wa silaha za kulipuka Yemen ndiyo kubwa zaidi duniani- OCHA

Idadi ya wahanga wa silaha za kulipuka Yemen ndiyo kubwa zaidi duniani- OCHA

Idadi ya vifo na majereha kutokana na silaha za kulipuka nchini Yemen, ndiyo kubwa zaidi duniani, limesema Shirika la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA.

Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA, raia wapatao 4,500 waliuawa au kujeruhiwa kwa vilipuzi nchini Yemen katika miezi ya kwanza ya saba ya mwaka 2015.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuliko katika nchi nyingine yoyote ile, kwa mujibu wa OCHA na shirika moja la kibinadamu kutoka Uingereza, Action on Armed Violence.

Taarifa ya OCHA pia imesema kuwa asilimia 95 ya watu waliouawa au kujeruhiwa kwa silaha za kulipuka katika maeneo ya watu wengi, walikuwa raia, zaidi ya nusu ya idadi hiyo ikiwa katika mji wa Sana’a na maeneo jirani.