Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha na elimu ya watu Sahel vinadhulumiwa: Lanzer

Maisha na elimu ya watu Sahel vinadhulumiwa: Lanzer

Mratibu maalum wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Sahel Toby Lanzer amesema hali ya kibaindamu katiak ukanda huo inazorota kila uchao kufuatia vuguvugu la ugaidi linalotekelezwa na kundi la Boko Haram .

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Lanzer amesema janga hilo ndio linalokuwa kuliko yote Afrika akitolea mfano kuwa watu takribani milioni mbili na nusu wamefurushwa makwao na kutengana na familia zao.

Amesema nchini Nigeria watoto milioni moja nukta nne wamefurushwa makwao siku za hivi karibuni , shule 1200 zimeharibiwa. Amesema jamii za Cameron, Niger na Chad zinahitaji elimu ili kujebga nchi zao.

(SAUTI LANZER)

‘‘Tuko hapa Umoja wa Mataifa kufanya kila tuwezalo kukabiliana na athari za kibinadamu mathalani kupitia WFP ambao wanafanya kazi kwa karibu na shirika la dharura nchini Nigeria kusaidia.’’