Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lajadili CAR

Baraza la haki za binadamu lajadili CAR

Hii leo huko Geneva, Uswisi, Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa na mashauriano shirikishi kuhusu hali ilivyo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo wajumbe wameelezwa kuwa miezi ijayo itakuwa muhimu sana katika kuamua mustakhbali wa nchi hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Wajumbe walipata taarifa kutoka kwa mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu CAR Therese Keita Boucoum ambaye pamoja na kutaja hatua chanya za serikali kurejesha utawala wa sheria na kuhakikisha uchaguzi unafanyika ilivyopangwa, amesema kuzidi kudorora kwa hali ya usalama nchini humo kunaweka mashakani harakati za uchaguzi.

Bi. Keita-Boucoum amesema kudorora kwa hali ya usalama kunahitaji hatua za dharura za kurejesha mashauriano baina uya jamii na kuzuia kuendelea kwa ghasia za kidini na kikabila.

Naye Mwakilishi wa CAR kwenye mkutano huo amekiri kudorora kwa usalama tangu tukio la tarehe 26 na 27 mwezi huu akisema wako tayari kushirikiana na Umoja wa Mataifa na wadau wengine kusitisha ghasia ili amani na utulivu virejee nchini humo.