Machafuko Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika yanazima ndoto za vijana: Ban
Baraza la usalama leo limekutana katika mjadala kuhusu utatuzi wa machafuko Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika pamoja na kupambana na vitisho vya ugauidi katika kanda hizo. Taarifa ya Amina Hassan imesheheni
(TAARIFA YA AMINA)
Mkutano huo umehudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali hususani zinazoguswa kwa namna moja au nyingine na machafuko katika nchi hizo.Katibu Mkuu wa UM Ban ki-moon amehutubia baraza hilo akisema jumuiya ya kimaataifa inawajibika kuchukua hatua dhidi ya uvunjaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaoendelea kutokana na machafuko katika nchi za Maahariki ya kati hususani Syria
Ban anasema kile amabacho kinatokea ikiwa machafuko yataendelea bila kudhibitiwa.
(SAUTI BAN)
‘‘Migogoro, kushindwa kuidhibiti na mfulululizo wa uvunjaji wa haki za binadamu yanaathiri sio tu Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika bali dunia kwa ujumla. Wanawake na wasichana wanakabiliwa na ukatili . Vijana wanappokonywa mustakabali wao kabla ya kupata fursa ya kutimiza ndoto zao.’’
Kwa upande wake kiongozi wa mkutano huo wa baaraza la usalam, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema ni muhimu kudhibiti ufadhili wa kifedha wa ugaidi.