Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Sirleaf ashukuru waliochangia katika kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

Rais Sirleaf ashukuru waliochangia katika kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

Rais was Liberia, Ellen Sirleaf Johnson amesema katika  kutafakari kuhusu nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwa na homa ya Ebola ambazo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone, imani ya kimsingi ya Umoja wa Mataifa imedhihirika, kwamba dunia inaweza daima kwa kupitia ubinadamu kukabiliana na hata maadui wasiotambuliwa na wanaotishia maendeleo ya pamoja.

Rais Sirleaf amesema hayo wakati wa hotuba yake kwa Baraza Kuu la Sabini la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Sambamba na hayo, Sirleaf amesema ni lazima kuwawashukuru wote kwa msaada wao katika kukabiliana na Ebola, tishio alillolitaja kuwa changamoto kubwa ya kisasa ya afya ya umma ya kimataifa.

Kuhusu usaidizi wa kupambana na Ebola, Rias Sirleaf amesema

(SAUTI ELLEN JOHNSON SIRLEAF)

Tunamshukuru Katibu Mkuu Ban ambaye kwa kushirikiana na nchi zetu na msaada kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia, wenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Ebola katika kuelekeza nguvu  pamoja na kutafuta msaada baada ya mlipuko wa Ebola”

Kuhusu nafasi ya wanawake katika Umoja wa Rais Sirleaf amesema

"Mwaka huu, tumeaadhimisha miaka ishirini ya kihistoria ya baada ya Mkutano  wa Beijing Mkutano na Mpango wake wa Utekelezaji wa uwezeshaji wa wanawake na Usawa wa  jinsia.  Pia tunadhimisha miaka 15 ya azimio la 1325  ya ushiriki wa wanawake katika michakato ya amani "