Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwaherini, Tanzania itasalia mwanachahama mwaminifu wa UM: Kikwete

Kwaherini, Tanzania itasalia mwanachahama mwaminifu wa UM: Kikwete

Nawaaga lakini Tanzania itasalia mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa. Ni sehemu ya hotuba ya mwisho kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliyotoa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake wa uongozi wake baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwake mwezi ujao wa Oktoba.

Katika hotuba yake Rais Kikwete amegusia masuala mbali mbali ikiwemo operesheni za ulinzi wa amani, masuala ya afya ikiwemo mlipuko wa Ebola na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kuepusha janga la aina hiyo pamoja na maendeleo.

Muda mfupi baada ya kumaliza kulihutubia baraza hilo Rais Kikwete amemweleza Joseph Msami wa idhaa hii katika mahojiano maalum kuhusu umuhimu wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI KIKWETE)

Kuhusu operesheni za ulinzi wa amani kiongozi huyo ambaye nchi yake imepeleka vikosi vya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan, anasema.

(SAUTI KIKWETE)