Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wajadili amani kwenye ukanda wa maziwa makuu

Umoja wa Mataifa wajadili amani kwenye ukanda wa maziwa makuu

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, kumefanyika mkutano wa sita wa kikanda kuhusu mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ukanda wa maziwa makuu, ukiangazia makubaliano ya amani, ulinzi na usalama yaliyopitishwa mwezi Februari mwaka 2013 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  amegusia umuhimu wa amani na usalama akigusia suala la uchaguzi unaokaribia kwenye baadhi ya nchi za ukanda huo.

(Sauti ya Ban)

“Baadhi ya nchi kwenye ukanda wa maziwa makuu zinatarajia kufanya uchaguzi muhimu. Nasihi serikali na viongozi kuwajibika kwa ajili ya wananchi kwa kuheshimu katiba zao za kitaifa pamoja na mkataba wa Afrika kuhusu demokrasia, uchaguzi na utawala. Uchaguzi ni hatua muhimu kwenye demokrasia changa. Tunapaswa kuhakikisha nchi za ukanda huo zinatoka na nguvu na ushirikiano zaidi kutokana na utaratibu huo.”

Jean-Christophe Belliard, Mkuu wa idara ya ukanda wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ambaye naye alishiriki mkutano huo amesema tatizo la ukanda wa Maziwa Makuu ni mzozo unaosahaulika.
Akihojiwa na Idhaa hii kabla ya kikao hicho amesema Ufaransa inasikitishwa na vurugu inayoendelea mashariki mwa DRC, licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO.

(Sauti ya Belliard)

Aidha amemulika hali ya vurugu nchini Burundi akitoa wito..

(Sauti ya Belliard)