Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama liwe shirikishi: Rais Mutharika

Baraza la usalama liwe shirikishi: Rais Mutharika

Rais wa Malawi Peter Mutharika amelihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa 70 ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa muundo shirikishi wa baraza la usalama .

Amesema mundo huo mpya wa baraza hilo uwe na ufanisi, wa uwazi na wenye kuwajibika. Rais Mutharika akazungumzia masuala ya amani na usalama.

(SAUTI MUTHARIKA)

‘‘Harakati zetu za amani na usalama lazima zilenge katika maendeleo endelevu ya kijamii na kichumi kwa ajili ya watu wetu , maendeleo ambayo yana maana halisi na yana akisi maisha ya watu wetu.’’

Kadhalika Rais huyo wa Malawi amesema malengo ya maendeleo ya milenia MDGS yaliyofikia ukomo wake yamethibitisha kuwa umoja katika lengo ni muhimu katika kuleta mabadiliko duniani.