Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa UNICEF asihi wakimbizi na wahamiaji Ulaya wapewe ulinzi

Balozi mwema wa UNICEF asihi wakimbizi na wahamiaji Ulaya wapewe ulinzi

Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Orlando Bloom ametoa wito wa ulinzi zaidi kwa maelfu ya watoto wakimbizi na wahamiaji kadri wanavyoendelea na safari zao Ulaya.

Katika taarifa, Bloom amesema wakati wa ziara yake kwa kituo cha kuwapokea wakimbizi cha Gevgelija, nchini Macedonia, kinachopakana na Ugiriki.

Bloom alisikiliza hadithi za safari zao hatarishi, matatizo yao sawa na matumaini yao ya siku za usoni.

Wengi wa wakimbizi na wahamiaji hao wamekimbia ghasia nchini Syria, Afghanistan na Iraq.

Bloom amesema, watoto hao wamesafiri njia hatarishi zaidi kwa wakimbizi na wahamiaji duniani, na alipozungumza na watoto hao ambao wamesafiri safari hiyo ya kutisha, mara nyingi katika hali ya hewa iliyo mbaya, wakitembea kwa viatu na nguo tu walizokuwa wamevaa.