Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola tumeshinda tunashukuru marafiki zetu: Rais Koroma

Ebola tumeshinda tunashukuru marafiki zetu: Rais Koroma

Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amehutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akigusia masuala ya mabadiliko ya tabianchi, amani, usalama, usawa wa kijinsia na ugonjwa wa Ebola ambao ulitikisa nchi yake.

Mathalani kuhusu mabadiliko ya tabianchi amesema hakuna nchi ambayo inaweza kukwepa athari za kijamii, kiusalama na kiuchumi zinazosababishwa na mabadiliko hayo.

Kwa mantiki hiyo amesema ni vyema kuzingatia hatua za kushughulikia mabadiliko hayo pindi viongozi wanapopitisha maamuzi kuhusu ukosefu wa ajira, usalama, njaa na usawa wa kijinsia.

Kuhusu Ebola, ugonjwa huo umekuwa na madhara makubwa katika mfumo wa kijamii na kiuchumi nchini Sierra Leone…

(Sauti ya Koroma)

“Lakini kutokana na usaidizi wa marafiki zetu, tumeshinda. Leo tumeshinda kirusi hiki kibaya, mwezi Agosti tulikuwa na kisa kimoja tu cha Ebola. Na kwa mwezi huu wa Septemba hatuna kisa chochote.”