Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye #UNGA, Rais wa Rwanda azingatia usawa katika uongozi wa kimataifa

Kwenye #UNGA, Rais wa Rwanda azingatia usawa katika uongozi wa kimataifa

Jukumu la Umoja wa Mataifa ni la msingi katika kukabiliana na changamoto za kisasa zikiwemo uhamiaji, mabadiliko ya tabianchi na utawala bora, amesema leo Rais wa Rwanda Paul Kagame akihutubia kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, mabadiliko ya uongozi yanahitajika katika ushirikiano wa kimataifa ili kufanikiwa katika hayo na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, amesema, akitaka usawa baina ya nchi ukuzwe zaidi.

Rais Kagame ameeleza kwamba tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa nchi za kiafrika zimetawaliwa bila kuwa na uwezo wa kupaza sauti zao, akisema mpaka sasa hivi sheria za kimataifa hazilazimu nchi zilizoendelea kama nchi zinazoendelea, akichukua mfano wa mapokezi ya wahamiaji barani Ulaya.

Akiongeza kuwa baadhi ya nchi wanapitia mashirika ya kimataifa kuhalalisha mashambulizi yao, amesema

(Sauti ya Rais Kagame)

“Hakuna nchi wala mfumo ambao una uhodhi wa busara, wala kudai kuongoza katika maadili. Jukumu letu ni kushughulikia yaliyo mbele yetu na si yaliyopita. Mabadiliko yanakuja, na ni ya lazima. Hakuna mmoja anayeweza kuyashughulikia pekee yake, na malengo ya maendeleo endelevu yanatambua kwamba tunategemeana sisi sote.”