Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa fedha si kitu, muhimu kuendeleza rasiliamli watu na kuaminiana: Rais Nyusi

Uhaba wa fedha si kitu, muhimu kuendeleza rasiliamli watu na kuaminiana: Rais Nyusi

Msumbiji ilipata uhuru wake mwaka 1975 kutoka Ureno na sasa iko katika harakati za kujikwamua kiuchumi na kijamii lakini vurugu za hapa na pale zinakwamisha mipango  hiyo wakati huu ambapo nchi hiyo imeungana na mataifa mengine kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Rais Felipe Nyusi wa Msumbiji, punde tu baada ya kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye mjadala wa wazi kuweza kufahamu hali ya amani na mustakhbali wa maendeleo. Lakini kwanza anaanza kwa kueleza ujumbe wake kwa Baraza Kuu.