Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika 12 ya UM yapaazia sauti haki za mashoga na wenye jinsia tofauti

Mashirika 12 ya UM yapaazia sauti haki za mashoga na wenye jinsia tofauti

Katika hatua ya kwanza ya aina yake, mashirika kumi na mawili ya Umoja wa Mataifa yametoa leo taarifa ya pamoja ikitoa wito wa kuchukua hatua kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na watu wanaojitambulisha kwa jinsia tofauti na muonekano wao, pamoja na barubaru na watoto. Taarifa kamili na Joshua Mmali

(Taarifa ya Joshua)

Taarifa hiyo ya pamoja inamulika uhusiano baina ya ukiukaji wa haki za binadamu za wapenzi wa jinsia moja na wanaojitambulisha kwa jinsia tofauti na muonekano wao, na afya mbaya, kusambaratika kwa familia, utengaji wa kijamii na kiuchumi na kupotea kwa fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.

Inaweka pia mwongozo wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali katika kuzuia ukatili na kuwalinda watu kutokana na ubaguzi, zikiwemo hatua za kuboresha uchunguzai na kuripoti kwa uhalifu wa chuki, utesaji, kuzuia ubaguzi na kufanyia marekebisho sheria zote zinazotumiwa kuwakamata, kuwaadhibu na kuwabaua watu kwa misingi ya mwelekeo wao kijinsia au wanavyojitambulisha.

Mashirika yaliyotoa taarifa hiyo ni lile la kazi, ILO, Ofisi ya haki za binadamu, UNAIDS, UNDP, UNESCO, UNHCR, UNFPA, UNICEF, UNODC, WFP na WHO.