Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Museveni ataka mabadiliko ya mifumo ya uchumi barani Afrika

Rais Museveni ataka mabadiliko ya mifumo ya uchumi barani Afrika

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amezingatia umuhimu wa ukuaji wa uchumi, viwanda, uwekezaji na biashara katika kuleta maendeleo kuliko misaada ya kibinadamu.

Akihutubia kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Museveni amesema mabadiliko ya uchumi barani Afrika ni jambo la msingi.

« Maendeleo endelevu bila mabadiliko ni kama kuzungumzia kiasi cha ukuaji wa uchumi bila mabadiliko bora. Jamii za kiafrika kwa mfano zinapaswa kukuwa kutoka kwa uzalishaji wa mali ghafi kwa jamii zenye utalaam na kipato cha kati. »  

Hatimaye kuhusu mizozo inayoendelea, Rais Museveni amesema anachopanda binadamu, ndicho anachovuna, akisema nchi zinazosambaza itikadi kali, chuki na ubaguzi, zitapata vita na vurugu.