Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatufahamu tumeikosea nini Marekani: Mugabe

Hatufahamu tumeikosea nini Marekani: Mugabe

Leo ni siku ya pili ya mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo viongozi mbali mbali wanatarajiwa kuhutubia akiwemo Rais Paul Kagame wa Rwanda na Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Hapo jana nyakati za jioni, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alihutubia akirejelea tena wito wa vikwazo dhidi ya nchi yake vilivyowekwa na Marekani na Muungano wa Ulaya vitolewe bila masharti yoyote na kwamba.

(Sauti ya Mugabe)

“Hatufahamu tumeikosea nini Marekani! Na je inaweza kutuachia huru ili tufanye mambo yetu tafadhali.”

Rais Mugabe amesema nchi yake sasa ina amani haitaki vurugu zozote iwe vita na hata harakati za kubadili serikali kwa maguvu akiongeza kuwa Zimbabwe inakaribisha marafiki hata wanaotofautiana ikiwemo Marekani na nchi za NATO.