Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la wakimbizi Ulaya limesababishwa na binadamu: Zuma

Janga la wakimbizi Ulaya limesababishwa na binadamu: Zuma

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaposhughulikia mizozo barani Afrika lihakikishe linasikiliza sauti za bara hilo na vyombo vyake vya kikanda badala ya kufanya vinginevyo.

Ni kauli ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alipohutubia mjadala wa wazi wa Baraza kuu akisema kuwa …

(Sauti ya Zuma)

“Hali ya sasa nchini Libya na ukanda wa Sahel ni matokeo ya moja kwa moja ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Usalama kutosikiliza wito kutoka Muungano wa Afrika. Wajibu wa kulinda ulitumika vibaya kwa maslahi madogo ya kisiasa ambayo hayana uhusiano kabisa na hoja ya msingi kuhusu mauaji ya watu wengi.”

Rais Zuma akaenda mbali zaidi kuhusu chanzo cha janga la wahamiaji na wakimbizi Ulaya..

(Sauti ya Zuma)

“Janga la sasa la wakimbizi Ulaya ni matokeo ya moja kwa moja ya kitendo cha kuwapatia raia silaha na vikundi vya upinzani huko Libya na Syria na nchi nyingine zilizoathirika. Kwa hiyo hili ni janga liilosababishwa na binadamu kwa makusudi.”