Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye meza ya chakula cha mchana, Ban awasihi viongozi wazingatie SDGs

Kwenye meza ya chakula cha mchana, Ban awasihi viongozi wazingatie SDGs

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, leo amekuwa na hafla ya chakula cha mchana na viongozi wa dunia, akiwaambia kwamba wanasherehekwa miaka 70 ya Umoja huo, ingawa pia wanafahamu kuwa ni wakati wa misukosuko. Ban amesema kuafikia na kupitishwa kwa malengo 17 ya maendeleo endelevu ni hatua ya kwanza ya kazi kubwa ya kufanya.

“Kama wanavyosema, hakuna chakula cha mchana cha bure. Natumai mtaweza kufanya yafuatayo. Tafadhali yapelekeni malengo nyumbani. Mwambieni kila mtu kuyahusu. Yaungeni kwa ushawishi wenu wa kisiasa, kwa kutunga sheria na juhudi za kitaifa. Yaungeni mkono kwa fedha. Mzimiliki SDGs na kuyafanya malengo vipaumbele vyenu.”

Aidha, Ban amesema vipaumbele vya viongozi wa nchi vitaleta mabadiliko.

“Yafanyeni yatimie. Haitakuwa rahisi. Mambo mengine yatashindana na umakinifu wenu. Lakini naamini kuwa matunda yake yatakuwa makubwa- kwanza kwa watu wenu na kwa dunia. Lakini pia kwenu binafsi.”