Kila mtu anasema lakini utekelezaji bado changamoto: Rais Nyusi

Kila mtu anasema lakini utekelezaji bado changamoto: Rais Nyusi

Rais Felipe Nyusi wa Msumbiji amesema maendeleo chanya yatokanayo na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa yanakabiliwa na ukungu kutokana na mizozo inayoendelea kukumba ulimwengu kwa sasa.

Akihutubia katika mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New  York, Marekani,  Rais Nyusi amesema mizozo hiyo inazidi kuathiri  binadamu na kwamba ni kiashiria kuwa Umoja huo umeshindwa kutoa hakikisho la amani na usalama duniani kwa mujibu wa malengo ya kuanzishwa kwake.

Alipohojiwa na Idhaa hii baada ya hotuba yake kuhusu nini kifanyike ili malengo ya kuanzishwa Umoja wa Mataifa yafanikiwe, Rais Nyusi amesema..

(Sauti ya Rais Nyusi)

Na kuhusu ujumbe wa Msumbiji kwa Baraza Kuu ni kwamba..

(Sauti ya Rais Nyusi)