Skip to main content

Ufadhili na Utashi wa kisiasa wahitajika kutimiza maendeleo Afrika: ripoti mpya

Ufadhili na Utashi wa kisiasa wahitajika kutimiza maendeleo Afrika: ripoti mpya

Uongozi, ubunifu na uwekezaji katika huduma za kijamii ndio zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia barani Africa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo mjini New York. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla )

Kwa mujibu wa ripoti hii iliyotolewa pamoja na Muungano wa Afrika, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa MDGs mwaka huu barani Afrika, mafanikio yamekuwa mengi katika kupunguza kiwango cha umaskini, ingawa bado asilimia 48 ya watu barani humo bado wanakumbwa na umaskini.

Licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika baadhi ya nchi, bado ukuaji wa uchumi, licha ya kuwa mkubwa kuliko sehemu nyingine duniani, hautoshi kuwapatia vijana wote ajira.

Ripoti imesisitiza kwamba ajenda ya mwaka 2063 ya Muungano wa Afrika pamoja na malengo 17 ya maendeleo endelevu yatawezesha Afrika kutokomeza umaskini iwapo utashi wa kisiasa na vyanzo vipya vya ufadhili vitapatikana.