Skip to main content

TEKNOHAMA yachangia maendeleo endelevu Tanzania: Rais Kikwete

TEKNOHAMA yachangia maendeleo endelevu Tanzania: Rais Kikwete

Uwekezaji katika Teknolojia za Habari na Mawasiliano, TEKNOHAMA umeleta mafanikio makubwa nchini Tanzania na inachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu amesema Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Idhaa hii.

Akihojiwa aye kabla ya kikao cha Shirika la Kimataifa la mawasiliano ITU ambapo tuzo mpya ya kumulika uongozi katika TEKNOHAMA imezinduliwa, Rais Kikwete amesema uwekezaji wa serikali katika sekta hiyo umesaidia kuinua maisha ya watanzania wengi.

(Sauti ya Rais Kikwete 1)

Aidha ameangazia sekta nyingine ya uwekezaji ya upatikanaji wa mtandao wa simu nchini kote.

(Sauti ya Rais Kikwete 2 )