Skip to main content

Mlinda amani wa UNAMID auawa, Ban alaani

Mlinda amani wa UNAMID auawa, Ban alaani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya mlinda amani mmoja wa ujumbe wa pamoja wa Umoja huo na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID.

Mlinda amani huyo kutoka Afrika Kusini aliuawa huku wenzake wengine wanne wakijeruhiwa wakati walipokuwa wakisindikiza msafara wa UNAMID uliokuwa umebeba vifaa huko Mellit, Darfur Kaskazini nchini Sudan.

Katika taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa Ban ametumba rambirambi kwa serikali ya Afrika Kusini na familia za mlinda amani huyo huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Halikadhalka amesihi serikali ya Sudan kuchunguza tukio hilo la Jumapili na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Ametoa wito kwa pande zote za mzozo huko Darfur kuheshimu maadili yanayolinda kikosi cha walinda amani akizikumbusha pande hizo kuwa zinaweza kuwajibishwa kwa mashambulio yoyote au vitisho dhidi ya UNAMI