Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu waanza leo

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu waanza leo

Mjadala wa wazi wa mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza leo kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani ambapo wakuu wa nchi na serikali wanaanza kuhutubia katika kikao hicho cha siku tatu.

Mjadala huu unafanyika baada ya siku tatu ya hotuba za viongozi zilizoanza Ijumaa baada ya kupitishwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs inayoweka mwelekeo wa mustakhbali wa dunia kwa miaka 15 ijayo.

Kwa mujibu wa ratiba, kikao kitaanza kwa hotuba kutoka kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye atawasilisha ripoti ya mwaka ya utendaji wa chombo hicho akifuatiwa na Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft ambaye atatoa hotuba rasmi ya ufunguzi.

Baada ya hotuba hiyo, wa kiongozi wa kwanza kuhutubia atakuwa Rais Dilma Rousseff wa Brazil akifuatiwa na Rais Barack Obama wa Marekani.

Viongozi wa Afrika Mashariki wanaotarajiwa kuhutubia leo ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Hotuba za viongozi zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia kiungo hiki cha televisheni ya mtandaoni ya Umoja wa Mataifa