Skip to main content

Tuwekeze katika elimu dhidi ya unyanyapaa kuutokomeza Ukimwi : Rais Mutharika

Tuwekeze katika elimu dhidi ya unyanyapaa kuutokomeza Ukimwi : Rais Mutharika

 Mapambano dhidi ya unyanyapaa kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na dhana potofu ni maeneo yakutilia mkazo ili kutokomeza ugonjwa huo amesema  Rais wa Malawi Peter Mutharika.

Rais  Mutharika ambaye alikuwa miongoni mwa watoa mada katika majadala uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la makabiliano dhidi ya Ukimwi UNAIDS, amemwambia Joseph Msami kandoni mwa mkutano huo kuwa elimu itawafanya watu wajitokeze na kupambana hadharani.

(SAUTI MUTHARIKA)

‘‘Tunahitaji rasilimali lakini  pia elimu ili kuukabili unyanyapaa, kwa mfano  watu wanafikiri fulani kaambukizwa virusi vya Ukimwi kwa kuwa hana tabia njema. Hili linawakatisha tamaa wengi, nchini Malawi angalau watu wameanza kujitokeza hadharani wakiwamo wanahabari mfano hivi karibuni mwandishi wa televeisheni alijitangaza na hakuathiri kazi yake. Tunapswa kuwa na mwenendo huo.’’

Hata hivyo amesema nchi za Afrika zinahitaji kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya Ukimwi licha ya ukosefu wa rasilimali.