Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna taifa lililo salama kutokana na mabadiliko ya tabianchi

Hakuna taifa lililo salama kutokana na mabadiliko ya tabianchi

Rais Mohamed Buhari wa Nigeria amesema ijapokuwa mataifa ya Bara la Afrika hayajachangia pakubwa kwa viwango vya joto duniani, hakuna taifa lililo salama kutokana na mabadiliko ya tabianchi huku akiongeza mataifa yaliyoendelea pia hayataepukana na mzigo wa mabadiliko hayo.

Kiongozi huyo amesema nchini Nigeria wameshudia mabadiliko ya hali ya hewa, kupanda kwa viwango vya usawa wa bahari, kusongea kwa jangwa, mvua nyingi, maporomoko ya ardhi na mafuriko, yote haya yakitishitia mzingira.

Halikadhalika, Rais Buhari amesema, hali hii sio tu inaathiri uhakika wa chakula, lakini pia maisha na uhai wa binadamu.

Rais Buhari amesema, matokeo ya makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi ya mkutano wa viongozi wa dunia mjini Paris, Ufararansa ni lazima yawe na msingi wa kisheria, yatabirike, na imara ili kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo.