Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia itatekeleza sheria itakayowanyima rufaa wanaowabaka wanawake- Rais Sirleaf

Liberia itatekeleza sheria itakayowanyima rufaa wanaowabaka wanawake- Rais Sirleaf

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, amesema leo kuwa serikali yake imepiga hatua katika kuongeza usawa wa jinsia, lakini akakiri kuwa bado kuna mapengo mengi, yakihitaji juhudi zaidi.

Kwa mantiki hiyo, Rais Sirleaf ameahidi kuwa serikali yake itahakikisha kuwa mswada ulioko bungeni sasa kuhusu ukatili wa majumbani unapitishwa ili kuulinda usalama wa wanawake.

Serikali yangu itaendelea kutekeleza sheria inayowanyima dhamana watu wanaotenda uhalifu wa ubakaji, ili kuhakikisha ulinzi bora zaidi wa wanawake wetu.”

Aidha, Rais Sirleaf ametoa ahadi kuhusu kutokomeza ukeketaji

“Serikali yangu inaahidi kuendeleza juhudi za kuwasilisha mswada katika bunge, wa sheria ya kuhakikisha upigaji marufuku na kutekeleza marufuku dhidi ya ukeketeji wa wanawake.”

Na kuhusu wanawake wanaofanya kazi katika sekta isiyo rasmi

“Serikali yangu inaahidi kuboresha mazingira ya maisha na kazi ya wanawake katika sekta isiyo rasmi, ambao huhakikisha uthabiti wa uchumi wetu, na ambao wametelekezwa zaidi."