Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya nyuklia yameweka mazingira bora ya ushirikiano. Dkt. Rouhani

Makubaliano ya nyuklia yameweka mazingira bora ya ushirikiano. Dkt. Rouhani

Mchakato wa miaka miwili sasa kati ya Iran na nchi sita zikiwemo tano wanachama watano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha kuna makubaliano kuhusu masuala ya nyuklia, uweka mazingira bora ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Hayo yamesemwa na Rais Hassan Rouhani wa Iran alipohotubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa jijini New  York, Marekani kuhusu ajenda mpya ya maendeleo endelevu, SDGs.

Amesema makubaliano hayo yameweka mazingira ya ushirikiano katika nyanja mbali mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira.

Dkt. Rouhani amesema mazingira ni suala nyeti ambalo linapaswa kuzingatiwa kwa kuwa mabadiliko ya tabianchi katika ukanda mmoja yanaathiri ukanda mwingine.

Amesema tayari Iran imechukua hatua kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa kuanzisha mitaala ya mazingira shuleni na kuangalia upya sera za ujenzi wa mabwawa huku wakihifadhi maeneo oevu.

Rais huyo wa Iran ametumia hotuba hiyo pia kutoa pole kwa familia za mahujaji waliofariki dunia Saudi Arabia wakati wa Hija, akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi huku akisihi uchunguzi ufanyike juu ya chanzo cha kisa hicho.