Skip to main content

Kufanikisha SDGs, China kuongeza msaada hadi dola Bilioni 12 ifikapo 2030

Kufanikisha SDGs, China kuongeza msaada hadi dola Bilioni 12 ifikapo 2030

Maendeleo  ambayo China imeshuhudia katika miongo kadhaa yameleta ustawi siyo tu kwa wananchi wake bali pia kwa wakazi wa maeneo mbali mbali dunia.

Amesema Rais Xi Jinping wa China wakati akihutubia katika siku ya pili ya mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, yaliyopitishwa Ijumaa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mathalani amesema kwa kipindi cha zaidi ya miaka Sitini China imechukua hatua za dhati za ushirikiano wa kimaendeleo kwa kupatia nchi 166 na mashirika ya kimataifa misaada yenye thamani ya karibu dola Bilioni 400 pamoja na wafanyakazi wa misaada.

Rais Xi amesema katika kusaidia nchi zinazoendelea kutekeleza SDGs, China itaanzisha mfuko maalum wa usaidizi wa ushirikiano wa nchi za Kusini ukiwa na fungu la awali la dola Bilioni Mbili na lengo ni kufikisha msaada wake kwa nchi hizo hadi dola bilioni 12 ifikapo mwaka 2030 na kwamba..

(Sauti ya Xi)

“China itasamehe madeni yake yote yasiyo na riba ambayo yalikuwa yalipwe ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2015 na nchi husika.Na misamaha hiyo ni kwa zile  nchini maskini, nchi zisizo na bandari nchi za visiwa vidogo.”