Tumepiga hatua muhimu katika kuinua wanawake Tanzania: Kikwete

Tumepiga hatua muhimu katika kuinua wanawake Tanzania: Kikwete

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amezungumza katika mjadala kuhusu kupambana na ukosefu wa usawa na kuwezesha wanawake na wasichana ikiwa ni sehemu ya malengo ya maendeleo enedelevu SDGs uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na ukiongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Katika mjadala huo Rais Kikwete amesema ni muhimu kufikia usawa wa kijinsia akiangazia elimu kwa watoto wa kike na usawa katika uongozi.

Kandoni mwa mkutano huo amemueleza mwandishi wa idhaa hii Joseph Msami Tanzania imefikia wapi katika kukuza usawa wa kijinsia.

(SAUTI KIKWETE)

Lengo namba tano la maendelo enedelevu SDGs linahusu kufikia usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake na wasichana, likijulikana kupitia alama ya reli #Planet5050.