Skip to main content

Utu na ujumuishwaji muhimu katika kufanikisha SDGS: Rais Sirleaf

Utu na ujumuishwaji muhimu katika kufanikisha SDGS: Rais Sirleaf

Ajenda ya maendeleo endelevu SDGS itafanikiwa ikiwa ujumuishwaji, utu kwa wote na autolewaji wa fursa utazingatiwa amesema Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf wakati akihutubia mkutano wa 70 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York.

Hata hivyo Rais huyo wa kwanza mwanamke barani Afrika amesema ubia wa kimaendeleo unahitajika pamoja na ufanisi katika utekelzaji wa malengo hayo na akasisitiza

(SAUTI)

‘‘Pamoja waraka huu unahitaji makubaliano ya kimataifa katika lengo moja la kutowesha umaskini na njaa, kulinda sayari yetu na kufungua milango ya mafaniko kwa ajili ya manufaa ya watu kila mahali’’

Amesema historia imenadikwa kwa kupitisha agenda 2030 hatua aliyosema ni jukumu na changamoto ya kuhakikisha kizazi kijacho hakina umasikini na kina usalama wa kutosha.