Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda 2030 ni ya kila mtu: Ban

Ajenda 2030 ni ya kila mtu: Ban

Zaidi ya watu milioni 8 wameshiriki katika uundaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs wakipata fursa za kusikilizisha sauti zao, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mjadala maalum uliofanyika leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, baada ya kupitishwa rasmi kwa ajenda hiyo ya 2030.

Bwana Ban amesema tathmini ya mahitaji ya raia imesaidia ajenda ya mwaka 2030 kuwa jumuishi na shirikishi.

Halikadhalika amesema ili watu waendelee kushirikishwa kwenye utekelezaji wa SDGs, ni muhimu malengo hayo yaunganishwe kwenye sera za kitaifa,

(Sauti ya Ban)

“Leo tunaweza kuwaambia watu wote duniani kote, na watalaam kutoka maeneo yote ambao wameshiriki kwenye mjadala huo wa kimataifa kwamba tumewasikia. Serikali zenu zimewasikiliza. Ajenda hii ni yenu, ni ya kila mtu.