Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya siku ya amani duniani

Maadhimisho ya siku ya amani duniani

Ndoto ya amani i miongoni mwa kila mtu duniani lakini zaidi kwa vijana ambao wanaelezwa kuwa na nafasi kubwa katika kusongesha amani. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika siku ya amani duniani iliyoadhimishwa kote duniani Septemba 21.

Katika muktadha huo ujumbe wa video wa Ban unasisistiza umuhimu wa kuwekeza kwa vijana ili kukuza amani enedelevu pamoja na maendeleo amabyo ni dhana muhimu katika amani..

(SAUTI BAN)

‘‘Viongozi wapaswa kuwekeza kwa vijana wajenzi wa amani, wote twaweza kukuza amani. Asasi za kiraia, mashirika ya kidini, na mashirika yanaweza kusaidia kuwa na dunia yenye amani zaidi. Katika siku chache zijazo viongozi wa dunia watapitisha ajenda ya 2030 ambayo ni mapango wetu wa maendeleo endelevu. Pamoja twaweza kufanikisha ubia kwa amani na utu kwa wote’’.

Mataifa mbalimbali kadhalika yameadhimisha siku hii adhimu ambayo inaamasha shauku ya kuenzi amani na kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Nchini Burundi ambako hivi karibuni imeshuhudia machafuko ya kisiasa, siku hii adhimu haikuachwa nyuma. Tuungane na mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga kutoka Bujumbura kufahamu hali ilivyokuwa..

(PACKAGE KIBUGA)