Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yajipanga kwa janga la uhaba wa chakula Malawi

WFP yajipanga kwa janga la uhaba wa chakula Malawi

Shirika la mpango wa chakula duniani,  WFP linajipanga ili kuweza kutoa usaidizi wa kutosha kufuatia uhaba mkubwa wa chakula kuwahi kukumba Malawi katika kipindi cha muongo mmoja.

Taarifa ya WFP imesema hatua hiyo inatokana la Rais Peter Mutharika wa Malawi kwa jamii ya kimataifa wakati akizindua mpango wa kitaifa wa kushughulikia uhaba wa chakula nchini humo.Imeelezwa kuwa kutokana na mafuriko makubwa, mavuno madogo na ukame katika maeneo tofauti tofauti, watu zaidi ya Milioni Mbili nukta Nane watakuwa na njaa kuanzia msimu wa mwambo unaonza mwezi ujao hadi machi mwakani.

Mwakilishi wa WFP nchini Malawi Coco Ushiyama amesema tayari mgao wa vyakula muhimu umeanza kufanyika sambamba na kuwapatia fedha za ununuzi kwa mujibu wa mpango huo wa uokozi ambapo ameshukuru serikali ya Malawi kwa kuchangia tani Elfu 26 za chakula kutoka hifadhi yake ya chakula.

Hata hivyo amesema wanahitaji fedha zaidi kwani ombi la fedha limechangiwa kwa asilimia 25 tu.