Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Papa Francis ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Papa Francis ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mara baada ya kuzungumza na wafanyakazi, Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiwa na viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja huo kabla ya kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Priscilla)

Nats..

Muongozaji akitambulisha viongozi wa dunia kwenye ukumbi wa Baraza kuu juu la ujio wa Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kuwahutubia akiwa anawakilisha Holy See.

Ndipo Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft akasema shida ni nyingi sasa duniani na hivyo..

(Sauti ya Mogens)

“Umuhimu wa ukumbi huu kushughulikia majanga haya kwa kuonyesha uongozi na vitendo kwa imani ya mshikamano na mazungumzo hauwezi kusisitizwa zaidi.”

Hatimaye Papa Francis akahutubia akitambua umuhimu wa shughuli za Umoja wa Matifa kama mwanga katika giza la vita na umaskini.

Amesisitza umuhimu wa kutunza mazingira kwani yaliumbwa na mungu na hatimaye akataka kupambana na kutengwa kijamii

(Sauti ya Papa Francis)

“ Kutengwa kijamii na kiuchumi ni kukanusha ubinadamu na kukiuka haki zabinadamu na mazingira. Watu maskini zaidi ndio wanateseka zaidi. Ni wahanga wa utamaduni wa leo wa kutumia na kutupa inayoenea pole pole kote duniani siku hizi. "

Amesema Ajenda ya mwaka 2030 ni matumaini katika kupambana na matatizo hayo, akitoa wito kwa viongozi watikmize ahadi zao, akisisitiza pia umuhimu wa kuleta mabadiliko katika uwakilishi katika vyombo vya Umoja wa Mataifa ikiwemo Baraza la Usalama.