Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ethiopia na Senegal ni mfano wa mapinduzi ya viwanda Afrika:UNIDO

Ethiopia na Senegal ni mfano wa mapinduzi ya viwanda Afrika:UNIDO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda duniani, UNIDO Li Yong amesema Ethiopia na Senegal zimeonyesha mfano wa jinsi mipango ya uendelezaji viwanda inayobuniwa na nchi husika inaweza kuleta mapinduzi ya viwanda barani Afrika na hivyo kufanikisha ajenda mpya 2030.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kuelekea kupitishwa kwa malengo ya maendelevu, SDG hii leo, Bwana Li ametolea mfano Ethiopia akisema viwanda kama vile vya ngozi na vyakula vinatumia malighafi kutoka nchini humo na ubia na sekta binafsi umeimarika na kwamba..

(Sauti ya Li)

“Theluthi mbili ya waajiriwa ni wanawake, hususan wasichana! Kwa hiyo vijana wanaajiriwa, hivyo vinaleta fursa ya ajira kukiwa na suala la kuwezesha wanawake na ajira kwa vijana.”

Hata hivyo amesema kwa nchi za Afrika kuwa na mapinduzi ya dhati ya viwanda...

(Sauti ya Li)

“Tunahitaji kuona viongozi na serikali zilizojizatiti. Kama serikali hazina dira ya aina hiyo ni vigumu kuwaeleza jinsi ya kusonga mbele. Halikadhalika jamii ya kimataifa kuunga mkono ni muhimu.”