Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Australia

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Australia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mashauriano leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Julie Bishop, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.

Katibu Mkuu na waziri huyo wa Australia wamejadili kuhusu ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, na haja ya msingi ya kumulika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, Ban akiihimiza Australia iendelee kuongoza katika suala hilo.

Aidha, wamebadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kuhusu kufuatilia na uwajibikaji kuhusu ajali ya ndege ya MH17.