Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakaribisha tangazo la Ulaya kuongeza ufadhili kwa wakimbizi

UNHCR yakaribisha tangazo la Ulaya kuongeza ufadhili kwa wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa  la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha tangazo la baraza la Umoja wa Ulaya la kuongeza rasilimali kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Syria pamoja na kutoa hifadhi kwa watu 120,000.

Taarifa ya UNHCR inasema uamuzi wa baraza la haki na mambo ya ndani la Ulaya kuhifadhi watu 120,000 halitatua tatizo la wahamiaji na wakimbizi kabisa lakini ni mwanzo wa suluhu.

Kamishna Mkuu wa UNHCR António Guterres amenukuliwa akisema kuwa ni hatua muhimu kuelekea utatuzi wa tatizo lakini akaongeza kuwa kuna mengi ya kufanya ikiwamo maeneno ya kuingilia wakimbizi na wahamiaji barani Ulaya kuandaliw awa ajili ya kuwapokea, kusaidia kuwasajili na kuwakagua.

Kadhalika UNHCR imekaribisha tangazo la uhitaji wa fadha kwa ajili ya nchi zinazotoa uhifadhi.