Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo huko Makka, Ban atuma rambirambi

Vifo huko Makka, Ban atuma rambirambi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametuma salamu za rambi rambi kwa familia, jamaa na serikali za mamia ya mahujaji waliofariki dunia huko, Makka Saudi Arabia wakiwa hija.

Ban ametoa rambirambi hizo wakati wa mkutano wa mawaziri wa kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo.

Amewatakia pia ahueni ya haraka majeruhi wa tukio hilo akisema ni matumaini yake kuwa chini ya uongozi wa serikali ya Saudi  Arabia, watapatiwa usaidizi wa haraka.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa katika tukio hilo la leo watu zaidi ya 700 wamefariki dunia na wengine zadi ya 800 wamejeruhiwa wakati mahujaji walipokanyagana kwenye mji mtakatifu wa Makka wakitekeleza nguzo ya tano ya uislamu ambayo ni hija.